Tangaza Hapa Ad

HekaHeka

HEKAHEKA: Mke amkimbia mumewe kwa kukosa haki ya ndoa kwa miezi minne

on

Leo September 26 2016 kupitia hekaheka ya Clouds FM, Geah Habibu ametuletea Heka Heka kutokea Tanga ambapo inahusu tukio la Bibi harusi kuondoka kwa mumewe kwa madai ya kwamba mumewe hajampa haki yake ya ndoa tangu amuoe.

Kwa mujibu wa Bibi harusi huyo anasema mpaka sasa ni miezi minne imepita tangu aolewe lakini mume wake hajawahi kumpa haki ya ndoa kwa madai kwamba anaumwa hivyo hawezi kufanya chochote kwa wakati huu.

Geah Habib amezungumza na Bwana Harusi ili kujua ukweli wa jambo hilo……..

>>>’Mimi sikufichi sina matatizo yoyote na kama ningekua mgonjwa nisingeoa yule dada nikapoteza gharama zangu, ushawahi sikia mtu mgonjwa wa hayo masuala anaoa mke, umesikia wapi? mi nachojua mtu anaweza kuwa ana nguvu zake ila tu zinapungua na ni mambo ya kawaida mnakaa chini na mwenzio mnaongea mkashughulikia kwa wataalamu’. 

>>>’Yeye anatoka anasema bwana angu hawezi kabisa hana tendo la ndoa wakati hatuna tatizo lolote na kama lingewepo angesema siku ile ya ndoa kuwa siwezi mwenzangu anasambaza maneno kwamba wewe sio mume wangu na kwetu usije tena. nikamwambia sawa kama umedai talaka utainunua mnilipe gharama zangu zote niende nikatafute mke mwingine’:- Bwana Harusi

Unaweza kusikiliza full stori kwa kubonyeza play hapa chini

ULIKOSA SABABU ZA JOKATE KUENDELEA KUISHI NA WAZAZI MPAKA SASA HIVI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement