Tangaza Hapa Ad

HekaHeka

HEKAHEKA: Ugomvi wasabaisha kifo Kunduchi DSM, aliyeuawa alikuwa hataki ugomvi

on

October 25, 2016 Kupitia Leo Tena ya Clouds FM  Geah Habib ametuletea hii Hekaheka iliyotokea Kunduchi  Dar es salaam, ni kuhusu ugomvi wa vijana wawili uliosababisha kifo cha mmoja wao, Kijana aliyeuawa  inadaiwa alikuwa hataki ugomvi.

Geah Habib amezungumza na kaka wa marehemu ambaye yeye anasema hakuwepo kwenye tukio ila alipigiwa simu baada ya mdogo wake kwenda polisi…………..

>>>’nikamkuta dogo kakaa nje ya kituo cha polisi nikamuuliza vipi, ananiambia amepigwa, anataka kuongea jina la mtu aliyempiga anashindwa, dogo anaambiwa aingie ndani atoe maelezo anapiga hatua ya kwanza ya pili akaanguka chini, alikuwa hajatoka damu sehemu yoyote bali alikuwa na nundu nayo ilionekana hospitali’:- Kaka wa Marehemu 

hek

Siku ya tukio marehemu alimtembelea rafiki yake na kumuomba watoke kutembea ambapo wakakutana na kijana ambaye alianzisha ugomvi na Dan, Rafiki yake amesimulia……

>>>’Alikuja kunitembelea nilikuwa naumwa malaria baadae akaniambie twende tukatembee, baadaye Juma gandi akawa ameshuka kwenye GSM tulikuwa tumekaa pale chini, Juma akawa anamunyoosha kidole kwamba leo nimekupata, akawa anasema mdogo wako ana dharau sana ngoja nimuonyeshe, Dan akawa ananiambia wewe muache tu siku nyingi amekuwa akiniambia hivyo muache tuone atafanya nini, Juma akaingia kibanda cha chipsi akachukua kisu’;-Rafiki wa Marehemu

>>>Mimi na muuza chipsi tukawa tumefanikiwa kumnyang’anya kisu Juma, tukawa tumehama hiyo sehemu kumbe alivyoondoka akaenda kumuita rafiki yake, ananiambia nisimtetee, nikauliza kwa nini wanapigana, yeye anasema tu mdogo wako anadharau, akavuta kuni moja kwa kustukiza ilikuwa karibu akampiga Dan akaanguka chini, kuni ya pili ikanipata mimi ikawa imenitoboa’;-Rafiki wa marehemu

  Kusikiliza full stori, Bonyeza play hapa chini

ULIKOSA HII YA SHAA KUHUSU MIPANGO YAKE YA KUSAINI WASANII WAKE? BONYEZA PLAY HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement