Tangaza Hapa Ad

fB insta twitter

Utafiti wabainisha athari za kuwa na kinyongo

on

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.

Moja ya taarifa ambayo ipo kwenye magazeti ya leo ni pamoja na hii  kutoka gazeti la Mtanzania lenye kichwa cha habari, ‘Kinyongo kinasababisha kansa’

Utafiti uliofanywa nchini Marekani umebaini kuwa asilimia 61 ya magonjwa ya saratani yanasababishwa na tabia  za watu kushindwa kusamehe wenzao waliowakosea.

Daktari Michael Barry ndio aliofanya utafiti huo nchini humo, ambapo sasa ameanzisha kliniki ya matibabu ya kusamehe Forgiveness Therapy.

Anasema watu wengi hushindwa kuwasamehe wenzao, hali ambayo huwasababishia msongo wa mawazo. ”wanakua hawana amani moyoni, muda mrefu wanakua na msongo wa mawazo dhidi ya wale waliowakosea, mwisho hujikuta wakiugua maradhi haya ya saratani.

Daktari bingwa wa kutibu magonjwa ya akili na mihemko, Steven Standiford wa Marekani anasema suala hilo lina ukweli ndani yake. ”wengi hushindwa kuhimili hali ya kutosamehe lakini pasipo kujua kwamba hali hiyo kujiua mwenyewe , kwani huwasababishia kupatwa kwa maradhi mbalimbali.

Akizungumza na Mtanzania Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dk Julius Mwaiselage alisema anakubaliana na utafiti huo kwa kiasi fulani.

Katika utafiti wake , daktari huyo wa Marekani, Barry anaamini kupitia msamaha lolote linawezekana. Katika kitabu chake kipya kiitwacho ‘The Forgiveness Project’ (Mpango wa kusamehe) kinachoendelezea uvumbuzi wa ajabu wa jinsi ya kupambana na ugonjwa wa saratani, kuwa na afya njema na kuwa na amani. Dk. Barry anaelezea uchunguzi alioufanya juu ya umuhimu wa msamaha katika afya na unavyoweza kuleta tiba ya ugonjwa mkubwa kama saratani.

Source: MTANZANIA

Unaweza kupitia hapa habari nyingine kubwa kutoka kwenye magazeti ya Tanzania leo September 24 2106

ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO TV SEPTEMBER 24 2016? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement