HekaHeka

HEKAHEKA: Mwendelezo Kichanga cha miezi miwili kilichopotea kimepatikana kiutata

on

Hekaheka ya leo January 15, 2018 nimuendelezo wa Hekaheka ya mtoto mchanga wa miezi miwili aliyepotea kwenye mazingira ya kutatanisha ambapo ilidaiwa kuwa hakuna mtu aliyefika kwenye nyumba hiyo wala mtu aliyetoka, kitu kilichosababisha wahusika kuhusisha na imani za kishirikina huku wakimtuhumu jirani yao kuhusika.

Sasa mtoto huyo amepatikana ni baaada ya mwanamke kumpeleka kwa siri na kumuweka karibu na nyumba ambayo alikuwa akiishi mtoto huyo huku akiwa amevalishwa nguo nyingine tofauti na zile ambazo alipotea nazo na mpaka mtoto huyo anarudishwa alikuwa katimiza siku nne.

Bonyeza PLAY kusikiliza ilivyokuwa..

Kichanga cha miezi miwili chapotea kiutata, anayedaiwa ataka yai iliamrudishe

Soma na hizi

Tupia Comments