Na ili kukuokoa kabla mambo hayajaharibika ni vema ukaanza kuandaa CV zako mapema. Nimekuwekea hapa dalili 10 za kugundua kama umechokwa ofisini kwako au na mwajiri wako na wanapanga kukuwashia moto.

  1. Majukumu Yasiyoeleweka: Mwanzo wakati unaanza kazi mambo yalikua safi lakini ghafla boss wako anaanza kukupangia majukumu mengine na ni yale ambayo anajua kabisa huna uwezo nayo au anakupa majukumu yasiyo na faida yoyote kwake na kwako!
  2. Haupewi nafasi ya kukutana na Boss wako. Muajiri wako anaanza kukukwepa au hakupi nafasi ya kuongea naye kama mwanzo, na hakupi majukumu yenye faida.
  3. Boss hapendi kukutana na wewe: Ni jambo la kushangaza inakuaje mtu aliyekua anakuamini sana ghafla inatokea hapendi kukutana na wewe iwe ni kwa issue za kiofisi au binafsi wakati mwanzo alikua anakushirikisha hadi mambo yake binafsi.
  4. Mipango au ushauri: Mwanzo ulikua mtu wa kwanza kuombwa ushauri na ulikua unaonekana ni wa maana sana unaanza kuonekana hauna nguvu wala ushawishi tena. Hauoni ushauri wako ukifanyiwa kazi kama mwanzo.
  5. Boss wako anatafua makosa: Vitu vidogo sana ulivyofanya vinakuzwa na unafokewa sana wakati mwingine unakua hata haujahusika.
  6. Unatakiwa kuwafundisha wengine: Sio jambo baya lakini ni la hatari inapotokea boss wako anaanza kukwambia uanze kuwafundisha watu wengine majukumu yako hasa waliokuwa chini yako. 
  7. Unajadiliwa sana kwenye vikao: Muda mwingi Boss wako anazungumza na HR kuhusu utendaji wa wafanyakazi na milango inakua imefungwa, ukiingia tu wananyamaza mpaka utoke.
  8. Haualikwi kwenye Vikao muhimu: Zamani ulikuwa wa kwanza kuambiwa chochote kuhusu vikao vya ofisi pamoja na maamuzi au mabadiliko yoyote ila sasa haushirikishwi kwa lolote.
  9. Unaombwa kuandika majukumu yako mara kwa mara: Ni jambo la ajabu sana, Boss wako ndiye aliyekupangia majukumu yako wakati unaajiriwa lakini ghafla anaana kukwambia umuandikie kazi unazofanya kila siku. Hapo anza kupanga vitu vyako. 
  10. Unatakiwa kueleza umefanya nini kwenye kampuni: Boss wako anakutaka umuandikie umefanya nini kwenye ofisi yake tangu ulipoajiriwa na unategemea kufanya nini kipya. 

ULIPITWA NA ALICHOKIZUNGUMZA MISS TANZANIA 2016 KABLA YA KUSHINDA TAJI HILO? NIMEKUWEKEA HAPA