Tangaza Hapa Ad

Michezo

Usitarajie kumuona Aguero akiichezea Argentina dhidi ya Uruguay na Venezuela

on

Chama cha soka cha Argentina AFA leo August 29 kimetangaza taarifa rasmi kuhusiana kukosekana kwa mshambuliaji wake anayeichezea Man City ya England Sergio Aguero katika list ya wachezaji watakaocheza michezo ya kuwania kufuzu kombe la dunia.

AFA wamethibitisha kuwa Sergio Aguero hatokuwemo katika kikosi cha wachezaji wa Argentina watakaocheza michezo miwili ya kuwania kufuzu Kombe la dunia dhidi ya timu ya taifa ya Uruguay na timu ya taifa ya Venezuele kutokana na nyota huyo kuwa majeruhi.

10aguero

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Aguero alikuwa sehemu ya kikosi cha Man City kilichocheza dhidi ya West Ham United weekend iliyoisha, lakini huo ndio mchezo uliyomfanya apate majeraha ya mguu wake.

GOAL AND HIGHLIGHTS: YANGA VS TP MAZEMBE JUNE 28 2016, FULL TIME 0-1

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement