Tangaza Hapa Ad

Michezo

Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya 9 leo kwa mwaka 2016

on

Staa wa soka wa kimataifa wa Ureno anayeichezea Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo anaumaliza mwaka 2016 kwa kufanikiwa kushinda tuzo yake ya 9 katika soka kwa mwaka 2016 baada ya leo kufanikiwa kushinda tuzo ya Globe Soccer Award akiwa Dubai.

Tuzo ya mwanasoka bora wa dunia wa Globe Soccer Award kwa mwaka 2016 inakuwa ni tuzo ya 9 kwa Ronaldo kwa mwaka 2016, baada ya kushinda tuzo za mchezaji bora wa Ulaya, The World Soccer, Four Four Two, EspyDi Stéfano Award, Goal.com award, FIFA Club Golden Ball na Ballon d’Or.

cristiano-ronaldo-globe-soccer-awards

Katika tuzo hiyo ya Globe Soccer Award 2016 Ronaldo alikuwa anawania na Lionel Messi, Jamie Vardy, Gonzalo Higuaín na  Antoine Griezmann, hii ni mara ya nne Ronaldo anashinda tuzo hiyo aliwahi kushinda 2011, 2013 na 2014.

Hata hivyo hivi karibuni pia Ronaldo alitangazwa kuwa mwanamichezo bora wa mwaka  Ulaya 2016 tuzo inayoandiliwa na vyombo vya habari 27 barani Ulaya, Ronaldo ndio mchezaji wa kwanza wa soka kuwahi kushinda tuzo hiyo.

ALL GOALS: JKT Ruvu vs Yanga December 17 2016, Full Time 0-3

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement