Tangaza Hapa Ad

Michezo

Ugo Ehiogu amefariki siku moja baada ya kuanguka uwanjani

on

Timu ya Manchester United leo imefuta mchezo wao wa wachezaji wa akiba dhidi ya wachezaji wa akiba wa Tottenham Hospurs kufuatia kufariki kwa kocha wa timu ya U-23 wa Tottenham Hotspurs Ugo Ehiogu, taarifa hizo zimetangazwa na Manchester United asubuhi ya leo April 21 2017.

Ugo Ehiogu ambaye alikuwa mchezaji wa zamani wa Aston Villa na timu ya taifa ya England amefariki leo Ijumaa ikiwa siku moja imepita baada ya kuanguka akiwa katika uwanja wa mazoezi wa Academy ya Tottenham Hotspurs kufuatia tatizo la moyo (cardiac arrest).

Beki huyo wa zamani wa Aston Villa na England amefariki akiwa na umri wa miaka 44, staa huyo amefariki na kuacha mke Gema na watoto Obi Jackson na Jodie lakini Ehiogu amefariki akiwa amewahi kuichezea Aston Villa zaidi ya mechi 300.

VIDEO: Game haikuoneshwa Yanga vs MC Alger, nimeyanasa matukio na goli la Yanga FT 1-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement