Tangaza Hapa Ad

AyoTV

VIDEO: Mahakama 20 za mwanzo kujengwa Dar es salaam

on

Waziri wa sheria na katiba Dkt Harrison Mwakyembe leo December 19 2017 alikutana na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ili kujadili mambo mbalimbali kuhusu mkoa wa Dar es salaam ikiwa ni pamoja na kumpongeza mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kwa jitihada mbalimbali ambazo amekuwa akizifanya.

Waziri mwakyembe amempongeza RC Makonda kwa juhudi zake mbalimbali hasa ikiwemo utafutaji wa vijana 35 ambao watakuwa wakitoa msaada wa kisheria bure kwenye mkoa wa Dar es salaam.

Baada ya serikali ya mkoa wa Dar es salaam kuanza na ujenzi wa vituo vya polisi 20, kingine ambacho kimeelezwa leo na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda mbele ya Waziri Mwakyembe ni kuwa kuanzia mwaka 2017 serikali ya mkoa wa Dar es salaam itaanza ujenzi wa mahakama za mwanzo 20 ili kuongeza kasi ya utoaji haki. Bonyeza play hapa chini kutazama

AyoTVMAGAZETI: Majaliwa ashtukia kifo cha Faru John, Taasisi zashtukiwa rushwa awamu ya tano, Bonyeza play hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement