Tangaza Hapa Ad

Michezo

PICHA 9: Yanga imechukua ushindi wa pili kanda ya ziwa leo

on

Jumatano ya October 19 Ligi Kuu soka Tanzania bara iliendelea kama kawaida kwa michez0 mitano kuchezwa huku mchezo wa sita wa Azam vs Mtibwa Sugar ukitarajiwa kuchezwa usiku wa leo katika uwanja wa Azam Complex Mbande Chamazi.

img-20161019-wa0033

Kwa upande wa Mabingwa watetezi Dar es Salaam Young Africans ilirudi kanda ya ziwa kucheza dhidi ya Toto Africans huku ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa goli 1-0 na Stand United siku kadhaa nyuma katika uwanja wa Kambarage Shinyanga, hiyo ilikuwa ni baada ya kuvuna point tatu dhidi ya Mwadui FC.

img-20161019-wa0049

Yanga wamerudi kanda ya ziwa safari hii kucheza dhidi ya Toto Africans na wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0, magoli ambayo yalifungwa na mzambia Obrey Chirwa dakika ya 28 na goli la pili lilifungwa na Simon Msuva dakika ya 55 kwa mkwaju wa penati, Obrey Chirwa leo anakuwa kafunga goli lake la pili akiwa na Yanga.

img-20161019-wa0037

img-20161019-wa0032

img-20161019-wa0051

img-20161019-wa0043

img-20161019-wa0048

img-20161019-wa0041


ALL GOALS: Yanga vs Simba October 1 2016, Full Time 1-1

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement