Habari za Mastaa

Trace TV wanasema hizi ni nyimbo 5 bora duniani mwaka 2013, ya Afrika moja tu

on

Trace TV 1Trace TV ni kituo cha TV cha Ufaransa maarufu kwa burudani ambapo kwa miaka kadhaa sasa hivi kimeendelea kuchukua watazamaji wapya wapenda muziki kila siku kutokana na ubora wa muziki unaopigwa na wao, video kali kutoka kila kona ya dunia ambapo mpaka sasa ni Watanzania wawili tu ambao video zinachezwa na kituo hiki (Ay na Diamond)

Hii hapa chini ni list ya video tano zilizoshika kuanzia namba 5 mpaka 1 kwenye chati nzima ya nyimbo bora 30 kwa mwaka 2013 on Trace TV ambapo ya Africa ni moja tu, ya Mi casa wa South Africa ambayo ni namba 4.

Namba 5 ni Fine China ya Chris Brown.

4. Jika ya Mi casa wa South Africa ndio imemiliki namba 4.

3. Mkali Drake na single ya ‘started from the bottom’ ndio amemiliki hii namba

2.Blurred lines Robin Thicke ft T.I na Pharrell ndio imeshika namba mbili mazee

1. Trace TV wanakwambia kwao hii ndio single namba 1 kati ya zote 30 zilizoingia kwenye chati kuchuana ipi ilikua kali kwa mwaka 2013 >>> Daft Punk – Get Lucky ft Pharrell.

Tupia Comments