Tangaza Hapa Ad

Michezo

Mastaa wawili wa Ligi Kuu Tanzania bara tutakaowaona wakicheza AFCON 2017 Gabon

on

Mashabiki wa Ligi Kuu soka Tanzania bara kwa mwaka 2017 watapata nafasi ya kuona wachezaji wawili wanaotoka katika Ligi ya Tanzania wakizitumikia timu zao za taifa katika michuano ya mataifa ya Afrika 2017, michuano ambayo itafanyika Gabon.

aq

Vincent Bossou mwenye jezi ya njano

Michuano ya AFCON itaanza kuchezwa mwakani katika nchi ya Gabon lakini mashabiki Ligi Kuu Tanzania bara watapata fursa ya kuwaona Juuko Murshid wa Simba akiichezea Uganda The Cranes baada ya wiki hii, yeye aliichezea Uganda na kuiwezesha kufuzu AFCON kwa mara ya kwanza katika historia baada ya miaka 38.

juuko-shangilia-ura

Juuko Murshid

Staa mwingine atakayeonekana AFCON 2017 ni Vincent Bossou anayeichezea Yanga na timu ya taifa ya Togo, licha ya Bossou kuwa mchezaji pekee wa Ligi Kuu Tanzania bara aliyewahi kucheza Kombe la Dunia, mwakani ataonekana tena akiichezea Togo katika michuano ya AFCON.

group

Nchi zilizofuzu kucheza AFCON 2017 nchini Gabon

ALL GOALS: Simba vs AFC Leopard August 8 2016, Full Time 4-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement