Tangaza Hapa Ad

Michezo

Ushindi wa Simba dhidi ya Kagera, unaendeleza rekodi yao na Stand United

on

Ligi Kuu soka Tanzania bara msimu wa 2016/2017 umeendelea tena leo October 15 2016 kwa michezo mitano kupigwa katika viwanja mbalimbali Tanzania bara, katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam Simba waliikaribisha Kagera Sugar ya Bukoba kucheza mchezo wao wa tisa wa Ligi Kuu Tanzania bara.

img_4382

Wekundu wa Msimbazi Simba wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0, ushindi ambao unakuja siku mbili baada ya kuifunga Mbeya City kwa idadi hiyo ya magoli katika dimba la Sokoine, magoli ya Simba yalifungwa na Mzamiru Yasini dakika ya 43 kwa kichwa baada ya kutumia vyema kona iliyopigwa na Shiza Kichuya.

img_4392

Simba waliendeleza mashambulizi na dakika ya 75 Shiza Ramadhani Kichuya akapachika goli la pili kwa Simba kwa mkwaju wa penati, ushindi huo wa Simba unawafanya waendelee kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu kwa kufikisha point 23 wakati Kagera wakibaki na point zao 15, hadi sasa ni Simba na Stand United ndio wanashikilia rekodi ya kutopoteza mchezo msimu huu.

img_4390

ALL GOALS: Yanga vs Simba October 1 2016, Full Time 1-1

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement