Tangaza Hapa Ad

Michezo

Haijalishi Ronaldo atapenda au hatopenda, Xavi ana msimamo mmoja tu

on

Wiki kadhaa zimepita toka kuibuke na vita ya maneno kati ya nahodha wa zamani wa klabu ya FC Barcelona ya Hispania Xavi Hernandez na nahodha wa kimataifa wa Ureno anayeichezea Real Madrid Cristiano Ronaldo kutokana na kujibizana kupitia vyombo vya habari.

Mvutano wa Ronaldo na Xavi ulikuja baada ya Xavi kuhojiwa na kituo cha Radio Hispania na kueleza kuwa Messi ni bora kuliko Ronaldo “Ronaldo ni bora kwa muda wake tatizo kuna mchezaji bora zaidi, Ronaldo ni mchezaji mwenye uwezo sana lakini kwa mimi hakuna mlinganisho kati yake na Messi labda kama wewe ni shabiki wa Real Madrid”

cristiano-ronaldo-457-trying-to-steal-the-ball-from-xavi-hernandez-in-barcelona-vs-real-madrid-clasico-2010-2011

Xavi na Ronaldo

Baada ya maneno hayo kutoka Ronaldo baada ya mechi ya Osasuna alitoa majibu kuhusiana na wazo la Xavi “Xavi anacheza soka Qatar au ? mimi sijui lakini kila mmoja ambaye anataka akae ukurasa wa mbele katika gazeti lazima anizungumzie, sawa Xavi ameshinda kila kitu lakini sio Ballon d’Or”

October 4 2016 Xavi akiwa katika red carpet karudia tena maneno yake na kusema kuwa kwake hawezi kuomba msamaha “Bado nasimamia msimamo wangu tatizo la Ronaldo kuna bora zaidi yake, nimesikia kuwa hajapokea vizuri hilo lakini siwezi kubadilisha kitu, kweli sijashinda Ballon d’Or lakini haikunifanya nikose heshima, unafikiria nini ? niseme samahani hiyo sio kutoka kwa Xavi”

ALL GOALS: Yanga vs Simba October 1 2016, Full Time 1-1

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement