Inawezekana wewe ni mmoja kati ya watu wanaotaka kujua winga mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania aliyekuwa anaichezea klabu ya Free State ya Afrika Kusini Mrisho Ngassa atajiunga na klabu gani baada ya kuvunja mkataba na Free State.
Septemba 21 2016 Mrisho Ngassa ambaye wengi walikuwa wakihisi kuwa atajiunga na klabu ya Tanzania baada ya kuvunja mkataba wake wa miaka minne na Free State, amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea Fanja SC ya Oman.
Mrisho Ngassa anaripotiwa kuvunja mkataba na Free State ya Afrika Kusini na sasa yupo huru kujiunga na timu yoyote. pic.twitter.com/dTVha1QIc5
— millard ayo (@millardayo) September 1, 2016
Ngassa anaungana na mshambuliaji wa Simba Danny Lyanga ambaye nae amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea timu hiyo, Ngassa alivunja mkataba wa miaka minne na Free State August 25 2016 kabla ya taarifa kutoka Septemba 1 2o16 akiwa ameitumikia mwaka mmoja pekee.
ALL GOALS: Simba vs AFC Leopard August 8 2016, Full Time 4-0