Tangaza Hapa Ad

Michezo

DONEDEAL: Ngassa kamaliza ubishi kasaini Uarabuni

on

Inawezekana wewe ni mmoja kati ya watu wanaotaka kujua winga mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania aliyekuwa anaichezea klabu ya Free State ya Afrika Kusini Mrisho Ngassa atajiunga na klabu gani baada ya kuvunja mkataba na Free State.

Septemba 21 2016 Mrisho Ngassa ambaye wengi walikuwa wakihisi kuwa atajiunga na klabu ya Tanzania baada ya kuvunja mkataba wake wa miaka minne na Free State, amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea Fanja SC ya Oman.


Ngassa anaungana na mshambuliaji wa Simba Danny Lyanga ambaye nae amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea timu hiyo, Ngassa alivunja mkataba wa miaka minne na Free State August 25 2016 kabla ya taarifa kutoka Septemba 1 2o16 akiwa ameitumikia mwaka mmoja pekee.

gt5

Fanja SC anaongoza msimamo wa Ligi Kuu Oman akiwa kacheza mchezo mmoja hadi sasa

ALL GOALS: Simba vs AFC Leopard August 8 2016, Full Time 4-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement