Tangaza Hapa Ad

Michezo

Wenger kakubali ubahili sio ishu kamsajilii staa wa Ujerumani

on

Ni good news nyingine kwa mashabiki wa soka la England hususani mashabiki wa klabu ya Arsenal inayofundishwa na kocha mfaransa Arsene Wenger, saa chache baada ya Arsenal kukamilisha usajili wa Lucas Perez wametangaza kukamilisha usajili wa beki wa Ujerumani.

Arsenal wametangaza kukamilisha usajili wa Shkodran Mustafi kutokea klabu ya Valencia ya Hispania, Mustafi ni mchezaji wa sita kusajiliwa na Arsenal msimu huu baada ya Lucas Perez, Granit Xhaka, Rob Holding, Takuma Asano na Kelechi Nwakali.

gun__1472561891_Mustafi
Mustafi mwenye umri wa miaka 24 anajiunga na Arsenal akiwa ameichezea Valecnia jumla ya mechi 64 katika misimu yake miwili akiwa na klabu hiyo, bado dau la usajili halijawekwa wazi ila inaaminika kuwa Wenger kaacha ubahili na kutumia karibia na pound milioni 35 ili kumpata staa huyo.

GOAL AND HIGHLIGHTS: YANGA VS TP MAZEMBE JUNE 28 2016, FULL TIME 0-1

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement