Tangaza Hapa Ad

Michezo

Muendesha mashitaka kaomba Neymar ahukumiwe miaka miwili jela

on

Headlines za uhamisho wa Neymar mwaka 2013 kutoka Santos kujiunga na FC Barcelona zinazidi kuchukua headlines kila kukicha, leo November 23 2016 suala hilo limechukua headlines mpya baada ya muendesha mashitaka kuomba  Neymar na Rais wa zamani wa FC Barcelona Sandro Rosell wahukumiwe.

Muendesha mashitaka amemuomba jaji Jose Perals kumuhukumu Neymar miaka miwili na kumuhukumu Rais wa zamani wa FC Barcelona Sandro Rosell miaka mitano jela kwa kosa la rushwa na ukwepaji kodi katika uhamisho wa Neymar 2013.

84901

Sandro Rosell na Neymar

Hata hivyo klabu ya FC Barcelona itapigwa faini ya pound milioni 7.2 kwa kosa hilo pia, kama utakuwa unakumbuka vizuri Sandrol Rosell alijiuzulu nafasi yake ya urais wa FC Barcelona mwaka 2014 kufuatia tuhuma za uhamisho wa Neymar ambazo zimegubikwa na ujanja ujanja.

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement