Tangaza Hapa Ad

Michezo

PICHA: Lwandamina katambulishwa Yanga, kocha Hans kapewa majukumu mapya

on

Uongozi wa klabu ya Dar es Salaam Young Africans leo November 25 kupitia makamu mwenyekiti wake Frank Sanga, wamemtambulisha rasmi aliyekuwa kocha mkuu wa klabu ya Zesco United ya Zambia George Lwandamina kuwa kocha wao mkuu.

Lwandamina anakuwa kocha mkuu wa Yanga na kurithi nafasi ya mholanzi Hans van Pluijm, ambapo uongozi wa Yanga umeamua kumpangia majukumu mengine, kwa sasa Hans van Pluijm anakuwa mkurugenzi wa ufundi wa klabu akifanya kazi kwa kushirikiana na Lwandamina.

mich22

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Lwandamina alijiunga na Zesco United 2014 na ameipa mataji  mawili ya Ligi Kuu, Barclay Cup, Charity Shield na ameiongoza timu hiyo 2016 kufika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kabla ya kuamua kujiuzulu nafasi yake hiyo Zesco na kuja kusaini Yanga miaka miwili.

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement