Tangaza Hapa Ad

Michezo

VIDEO: Real Madrid imefuzu hatua ya nusu fainali Champions League

on

Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambayo inajulikana kama UEFA Champions League iliendelea usiku wa April 18 2017 kwa michezo miwili ya marudiano ya robo fainali kuchezwa, Leicester City walikuwa wenyeji wa Atletico Madrid ambapo Leicester City walitolewa kwa aggregate ya magoli 2-1.

Real Madrid wao walikuwa katika uwanja wao wa Santiago Bernabeu kucheza dhidi ya FC Bayern Munich ambako katika mchezo wa kwanza uliyochezwa Ujerumani Real Madrid alishinda kwa goli 2-1, leo Real Madrid wakiwa nyumbani wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 4-2, ushindi ambao ulipatikana ndani ya dakika 120.

Cristiano Ronaldo kwa mara nyingine tena anakuwa mchezaji hatari na kuleta madhara makubwa kwa kufunga hat-trick katika game hiyo, matokeo hayo yanaifanya Real Madrid na Atletico Madrid timu zinazotokea katika jiji la Madrid kufuzu hatua ya nusu fainali, huku FC Barcelona akisubiri kucheza na Juventus kesho na Dortmund kucheza dhidi ya AS Monaco.

Hat-trick ya Ronaldo ilimfanya atimize magoli 100 ya Champions League lakini ni magoli 103 kwa michuano ya Ulaya ngazi ya club

VIDEO: Game haikuoneshwa Yanga vs MC Alger, nimeyanasa matukio na goli la Yanga FT 1-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement