Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Kama umewahi kuitazama Isidingo, huyu ndio mwigizaji wao aliefariki jana.

on

letty 2Lesego Motsepe maarufu kama Letty Matabane ni staa wa tamthilia ya Isidingo ambae uigizaji wake kwenye sehemu kubwa ya tamthilia hiyo ambayo Watanzania wengi wamekua wakiifatilia kupitia ITV.

Taarifa iliyotolewa inasema kaka mtu ndio alimkuta Letty akiwa amefariki nyumbani kwake saa tano asubuhi January 20 2014 ambapo kifo chake kilithibitishwa saa kadhaa baadae.

Letti 1

Mwaka 2011 mwishoni Motsepe alitangaza hadharani kuwa amekua akiishi na virusi vya ukimwi kwa karibu miaka 13 na uamuzi huo wa kujitangaza alitaka kuleta mabadiliko na kuwasaidia wale wanaoishi kwenye aina hiyo ya maisha kama yake.

Pamoja na kwamba alijitangaza kuishi na virusi vya ukimwi, chanzo cha kifo chake hakijatangazwa bado.

Screen Shot 2014-01-20 at 9.44.32 PM

letti 3Ripoti hii imetolewa na Mail & Gurdian.

Screen Shot 2014-01-20 at 9.39.51 PM

Tupia Comments

Advertisement