Biko


Tangaza Hapa Ad

AyoTV

Alichoongea Rais Magufuli kwa Babu Seya na watoto wake Ikulu leo

on

Jumanne ya January 2 2017 mwanamuziki Nguza Vicking maarufu kama Babu Seya na watoto wake watatu Johnson Nguza (Papii Kocha), Francis Nguza na Michael Nguza walimtembelea Rais Magufuli Ikulu Dar es Salaam na kumshukuru kwa kuwatoa gerezani kwa msamaha wa Rais.

Rais Magufuli alitangaza kuwatoa gerezani wafungwa mbalimbali kwa msamaha wa Rais siku ya maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania December 9 2017 wakiwemo Papii Kocha na Nguza Vicking ambao leo wamefika Ikulu kumsaliamia.

Baada ya Rais Magufuli kukutana na Babu Seya na watoto wake leo na kupokea shukrani zao aliwaambia hivi “Nawashukuru unajua hata kule kushukuru tunaambiwa tushukuru kwa kila jambo mimi sikutegemea kama mtakuja kuniona niliyoyafanya haya sio mimi bali ni mipango ya Mungu, shukrani nyingi zimuendee Mungu”>>> Rais JPM

Video iliyowanasa Babu Seya na wanae wakiingia IKULU leo

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement