Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Huyu ndio Liverpool watamtangaza kuwa mbadala wa Coutinho

on

Baada ya saa kadhaa kupita toka club ya FC Barcelona ithibitishe kuwa imefanikiwa kumsajili staa wa Brazil kutokea club ya Liverpool ya England Philippe Coutinho, Liverpool wameripotiwa kuwa wapo katika hatua za mwisho za kumsajili staa wa Leicester City Riyad Mahrez.

Liverpool wameripotiwa kuwa January 7 2018 watamfanyia vipimo vya afya Riyad Mahrez raia wa Algeria na akifuzu vipimo hivyo watampa mkataba wa miaka minne wa kuitumikia Liverpool kwa ada ya uhamisho wa euro milioni 55.

Riyad Mahrez

Maamuzi hayo yanakuja ikiwa ni saa chache zimepita toka Liverpool waingize pound milioni 142 kwa kumuuza Coutinho ambaye Riyad Mahrez ndio wanamsajili kama mbadala wake, Liverpool walimsajili Coutinho mwaka 2013 akitokea Inter Millan ya Italia kwa pound milioni 8.5.

Philippe Coutinho

Good news aliyoitangaza Mbwana Samatta January 6 2017

Soma na hizi

Tupia Comments