Michezo

George Weah amemtumia mualiko kocha Arsene Wenger

on

Rais mteule wa Liberia George Weah leo Ijumaa ya January 5 2018 ameripotiwa kumtumia mualiko kocha wa club ya Arsenal ya England Arsene Wenger ili haudhuri shughuli ya uapishwaji wake, George Weah ambaye ataapisha hivi karibuni aliwahi kufundishwa na Wenger.

Kocha Arsene Wenger amethibitisha kuwa amepokea mualiko huo kutoka kwa George Weah ambaye ataapishwa mapema mwezi huu lakini bado hajawa na uhakika kama ataweza kuhudhuria shughuli za uapishwaji wake.

“Nimealikwa na George Weah kuhudhuria siku yake ya kuapishwa kuwa Rais wa Liberia, naamini nitakuwa bize sidhani kama nitaweza kuhudhuria lakini kama nitakuwa nimefungiwa kama alivyokuwa amependekeza refa nitakuwa na nafasi ya kwenda”>>>Wenger

Wenger aliwahi kumfundisha George Weah katika kipindi cha miaka minne kuanzia 1988-1992 wakati ambao Wenger alikuwa anaifundisha AS Monaco, George Weah hadi anastaafu soka yeye ndio mchezaji pekee kutokea Afrika aliyewahi kushinda Ballon d’Or 1995.

Simon Msuva amerudi Tanzania leo, alichozungumza kipo hapa

Soma na hizi

Tupia Comments