Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Weasel atakachokifanya London kwa mara ya kwanza baada ya kifo cha Radio

on

Ni siku 11 zimepita toka kitokee kifo cha Staa wa muziki kutoka kundi la Good Lyfe kutoka nchini Uganda Radio ambaye alifariki February 1, 2018 kufuatia shambulio lililomjeruhi maeneo ya kichwani wakati akiwa Club nchini kwao Uganda.

Kundi la Good Lyfe lilikuwa linaundwa na marehemu Radio na Weasel ambaye ni mdogo wa Legend wa muziki nchini Uganda Jose Chameleon, leo zimeripotiwa taarifa mpya kutoka mpasho kuhusu Weasel kuwa atafanya show kwa mara ya kwanza kama solo artist.

Good Lyfe crew baada ya kifo cha Radio wanatarajiwa kwenda London kufanya show ambayo ni kama sehemu ya kumuaga Radio, show hiyo inaripotiwa kuwa sasa Weasel ndio atakuwa anaperform kwa mara ya kwanza kama solo artist toka afariki Radio, Radio alifariki February 1, 2018 baada ya kulazwa mahututi kwa muda siku 10 kufuatia kujeruhiwa kichwani kutokana na kudaiwa kupigwa akiwa club.

Radio

Mtuhumiwa wa shambulio la Radio lililopelekea kifo chake Godfrey Wamala ameshakamatwa na yupo katika gereza la Kigo  kama mahubusu wakati huu upelelezi wa kesi yake ukiwa unaendelea ili kubaini ukweli wa tukio lenyewe.

Unaweza kutazama video ya mwisho ya Radio na Weasel waliyoitoa December 20 2017 ‘Remember Me’

xxxx

Soma na hizi

Tupia Comments