Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Mourinho amewatolea uvivu Ryan Giggs na Rooney

on

Kocha wa Man United Jose Mourinho leo ameamua kuwatolea uvivu mastaa wa zamani wa Man United Wayne Rooney ambaye kwa sasa anaichezea Everton na Ryan Giggs ambaye kwa sasa ni kocha wa timu ya taifa ya Wales.

Rooney na Giggs wote wamekosoa mfumo wa Jose Mourinho namna anavyomtumia kiungo wao Paul Pogba kwa sasa, Rooney amemuelezea kuwa Pogba ni kiungo mwenye uwezo wa kucheza box to box na anapaswa kucheza huru uwanjani wakati Giggs yeye amehoji nafasi anayomtumia Mourinho.

Jose Mourinho ameamua kujibu tuhuma hizo mbele ya waandishi wa habari “Nimechekeshwa sana na nilivyovisikia na kuviona wiki iliyopita, nilichanganyikiwa kidogo kuona comments za baadhi ya watu muhimu katika soka, watu wanasema ipi ni nafasi yake sahihi (Pogba), Paul ni mchezaji wa nafasi ya kiungo haijalishi timu inacheza kwa mbinu gani lakini Pogba ni kiungo>>>Jose Mourinho

VIDEO: Simba imetangaza kumpeleka Haruna Niyonzima India

Soma na hizi

Tupia Comments