Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Hivi ndivyo walivyorudi Simba kimataifa leo

on

Baada ya kutoshiriki michuano ya kimataifa kwa muda mrefu kwa club ya Simba, hatimae leo February 11 2018 Simba imerudi katika michuano ya CAF kwa kucheza game yake ya kwanza dhidi ya Gendermarie ya Djbout.

Simba leo imecheza game yake ya kwanza ya roud ya kwanza ya michuano ya Kombe la shirikisho Afrika dhidi ya Gendermarie katika uwanja wa Taifa Dar es salaam na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 4-0.

Magoli ya Simba leo yamefungwa na Said Hamis Ndemla dakika ya 1, John Bocco aliyefunga magoli mawili dakika ya 33 na 42 na Emmanuel Okwi baada ya kukosa nafasi kadhaa za wazi akafanikiwa kufunga goli la mwisho la Simba dakika za nyongeza, mara ya mwisho Simba kushiriki michuano ya kimataifa ilikuwa mwaka 2012.

VIDEO: Goli la Juma Mahadhi lililoikosoa Yanga vs St Louis uwanja wa Taifa

Soma na hizi

Tupia Comments