Tangaza Hapa Ad

Michezo

PICHA: Ajib na Mavugo ndio mashujaa wa Simba dhidi ya Mtibwa Sugar

on

Ligi Kuu soka Tanzania bara msimu wa 2016/2017 iliendelea tena leo Septemba 11 2016 kwa wekundu wa Msimbamzi Simba kuwakaribisha wakatamiwa wa Manungu Turiani klabu ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam kucheza mchezo wa nne wa Ligi Kuu Tanzania bara.

img_0201

Simba imeshuka dimbani kucheza Mtibwa Sugar ikiwa na kumbukumbu ya kuifunga goli 1-0 msimu uliopita nyumbani na ugenini, kabla ya leo Septemba 11 2016 kuibuka na ushindi wa tatu wa goli 2-0 na kufanya hicho kuwa kipigo cha tatu mfululizo kwa Mtibwa Sugar kufungwa na Simba katika VPL.

img_0213

Kipindi cha kwanza kilikuwa kigumu kwa timu zote mbili kabla ya kipindi cha pili Simba kuja na mbinu mbadala iliyoifanya Mtibwa kufungwa goli la kwanza dakika ya 52 kupitia kwa Ibrahim Ajib na baadae Laudit  Mavugo akafunga goli la pili dakika ya 66.

img_0205

img_0207

img_0208

Matokeo ya mechi nyingine ya VPL iliyochezwa leo Septemba 11 2016

  • Tanzania Prisons 1-0 Toto Africans 

ALL GOALS: Simba vs AFC Leopard August 8 2016, Full Time 4-0 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement