Tangaza Hapa Ad

Michezo

Misri imekuwa timu ya pili Afrika kufuzu Kombe la Dunia 2018, bye bye Uganda

on

Timu ya taifa ya Misri usiku wa October 8 2017 inaingia katika historia nyingine kwa kuwa timu ya pili kutokea Afrika kufuzu kucheza Kombe la dunia 2018 nchini Urusi kwa kuifunga timu ya taifa ya Congo Brazzaville kwa magoli 2-1, ushindi ambao ni pigo ukanda wa Afrika Mashariki tulipokuwa tunaitegemea Uganda.

Magoli ya timu ya taifa ya Misri yakifungwa na Mohamed Salah aliyefunga magoli mawili dakika 64 na dakika za nyongeza 90+5 kwa mkwaju wa penati hiyo ni baada ya dakika ya 87 Congo kusawazisha goli la kwanza kupitia kwa Arnold Bouka Mouttou, hivyo Misri walilazimika kusubiri hadi dakika za nyongeza kukata tiketi.

Ushindi huo sasa unaifanya Misri kuwa timu ya pili Afrika kukata tiketi ya kucheza Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi baada ya Nigeria kufuzu jana, Misri wanafuzu kutokana na kufikisha jumla ya point 12 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ile katika Kundi E, hiyo inatokana na Uganda jana kutoka sare tasa dhidi ya Ghana mchezo wa Kundi E.

Hadi sasa timu zilizofanikiwa kufuzu kushiriki michuano ya Kombe la dunia 2018 itakayochezwa nchini Urusi ni pamoja na Urusi ambaye ni mwenyeji, Brazil, England, Iran, Nigeria, Japan, Mexico, Costa Rica, South Korea, Saudi Arabia, Ujerumani, Hispania na Poland.

ALL GOALS: Taifa Stars vs Malawi October 7 2017, Full Time 1-1

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement