Tangaza Hapa Ad

Michezo

Mambo matano ya kufahamu kuelekea mechi ya Liverpool vs Man United

on

Usiku wa October 17 2016 klabu za Liverpool na Man United zitakutana kwa mara ya 192 katika historia lakini mchezo huo wa Ligi Kuu utakuwa ni mchezo wa 162 kukutana vilabu hivyo katika michezo ya Ligi Kuu. Mtu wangu wa nguvu kuelekea mchezo naomba nikusogezee takwimu za timu hizo.

1- Kwa ujumla Man United na Liverpool wamecheza jumla ya mechi 192, Man United wakishinda 78 na kufunga magoli 269, Liverpool wameshinda mara 63 na kufunga magoli 245 na wametoka sare 51.

2- Katika mechi za Ligi Kuu wamecheza mara 162, Man United wameshinda mara 64 na kufunga magoli 223 na Liverpool wameshinda mechi 53 na kufunga magoli 202 na wametoka sare mara 44.

3- Katika mechi 5 za hivi karibu za Liverpool wameshinda mechi zote tano na wamefunga kuanzia magoli 2 na kuendelea, wakati Man United wameshinda mechi 3, sare mechi moja na wamefungwa mechi moja.

4- Katika mechi zao tano za mwisho kukutana kwa Liverpol na Man United, yamefungwa jumla ya magoli 12, Man United kashinda mechi tatu na kapoteza mechi moja na sare mechi 1.

5- Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp toka amejiunga na klabu hiyo October 2015, Liverpool wamefunga jumla ya magoli 73, idadi ambayo inaifanya kuwa ndio klabu pekee iliyofunga magoli mengi EPL.

ALL GOALS: Yanga vs Simba October 1 2016, Full Time 1-1

 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement