Tangaza Hapa Ad

Michezo

Kama ni shabiki wa Barcelona usishangae ukimuona Coutinho Nou Camp

on

Staa wa Liverpool raia wa Brazil Philippe Coutinho mwezi July aliingia kwenye headlines baada ya tetesi za usajili kuhusisha jina lake kuwa anakwenda Hispania kujiunga na club ya FC Barcelona ya kama mbadala wa Neymar aliyekuwa anatazamiwa kujiunga na PSG.

Good News kwa mashabiki wa club ya Ligi Kuu England ni kuwa gazeti la Mundo Deportivo limeripoti kuwa uongozi wa Liverpool umeridhia kumuachia Coutinho ajiunge na club ya FC Barcelona ya Hispania ifikapo mwezi January.

Barcelona walituma ofa nono zaidi ya tatu kwa Liverpool kuwashawishi wamuachie Coutinho lakini haikuwa rahisi kumuachia, ila leo October 11 2017 gazeti la Mundo Deportivo la Hispania limethibitisha kuwa staa huyo ataondoka Liverpool mwezi January taarifa zimevujishwa na viongozi wa Barcelona.

List ya majina 30 ya wanaowania tuzo ya Ballon d’Or 2017

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement