Tangaza Hapa Ad

Michezo

Maamuzi waliyofikia vilabu vya soka Brazil, baada ya timu ya Chapecoense kupata ajali na kufariki

on

Moja kati ya habari za masikitiko leo November 29 2016 katika ulimwengu wa soka ni kuhusiana na taarifa za ajali ya ndege ya timu ya Chapecoense ya Brazil iliyotokea asubuhi ya leo November 29 Colombia  ikiwa inakaribia kwenda kutua.

Baada ya habari hizo kutoka na kufahamika kuwa watu 76 kati ya 81 waliokuwepo katika msafara huo kupoteza maisha, hivyo Chapecoense kupoteza wachezaji wake kwa asilimia kubwa, vilabu vya soka vya  Corinthians, Santos, Sao Paulo na Palmeiras vya Brazil vimeiomba FA ya Brazil maombi maalum.

1480397623_017517_1480398498_noticia_normal

Vilabu hivyo vimeiomba FA ya Brazil kuruhusu klabu ya Chapecoense kupokea wachezaji wengi bure na mkopo kwa mwaka 2017, la pili ni kuwa Chapecoense isishushwe daraja katika kipindi cha mpito cha miaka  mitatu wakiwa wanajenga timu yao, hata kama itakuwa imeshika nafasi za kushuka daraja, ikitokea hivyo aliyejuu yake atashushwa daraja.

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement