Tangaza Hapa Ad

AyoTV

VIDEO: Kocha wa Azam FC ametaja alipowaweza Yanga na kuwafunga goli 4-0

on

January 7 2017 historia mpya imeandikwa katika ardhi ya Zanzibar baada ya Azam FC kuifunga Yanga kwa goli 4-0, mara ya mwisho Yanga kufungwa idadi kubwa ya magoli ilikuwa 2012 dhidi ya Simba alifungwa goli 4-0.

Baada ya mchezo kocha wa Azam FC alinaswa na vipaza sauti vya waandishi wa habari na moja kati ya maswali aliyolazimika kuyajibu kwa mtazamo wake anaamini Yanga walikosea wapi hadi akafanikiwa kuwafunga goli 4-0.

“Yanga wanategemea sana mipira ya pembeni sasa kwa kuwa wanategemea sana mipira ya pembeni tumejaribu kuwaangalia wale watu ambao wanawachezesha wale watu wa pembeni tukaona tukiwakamata sehemu ya kiungo unakuwa umeua lengo lao”

VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement