Tangaza Hapa Ad

Michezo

Baada ya vipimo Coutinho atakuwa nje kwa wiki 6, hizi ndio mechi atakazozikosa

on

Mchana wa November 28 2016 kiungo mshambuliaji wa Liverpool Philippe Coutinho alipelekwa hospitali na alifanyiwa vipimo vya afya vya mwisho, ili kujua jeraha lake la kifundo cha mguu litamuweka nje ya uwanja kwa muda gani.

p161126-024-liverpool_sunderland

Kiungo huyo wa kibrazil taarifa ya vipimo vyake imetoka na atakuwa nje ya uwanja kwa wiki 6 kufuatia kuumia kifundo cha mguu, Coutinho aliumia katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Sunderland, uliyochezwa Jumamosi ya November 26 na kumalizika kwa Liverpool kuibuka na ushindi wa goli 2-0.

photogrid_1480355306339

Liverpool watamkosa staa huyo katika michezo 7 ya Ligi Kuu England, mechi ambazo Bournemouth (Dec 4), West Ham (Dec 11th), Middlesbrough (Dec 14th), Everton (Dec 19th), Stoke City (Dec 27), Man City (Dec 31) na Sunderland (Jan 2), Coutinho anatazamiwa kurudi uwanjani January 15 2017.

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement