Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Man City ilivyorudi kwenye kasi yake leo January 2 2018

on

Usiku wa Janury 2 2018 michezo minne ya Ligi Kuu England msimu wa 2017/2018 ilichezwa katika viwanja mbalimbali na Man City wao ambao wiki iliyopita walipunguzwa kasi yao kwa sare tasa dhidi ya Crystal Palace wamerudi mchezoni kwenye game ya leo dhidi ya Watford.

Man City wakiikaribisha Watford katika uwanja wao wa Etihad na kufanikiwa kuwafunga Watford kwa magoli 3-1, magoli ya Man City yakifungwa na Raheem Sterling sekunde ya 38, Kabasele aliyejifunga dakika ya 13 na Sergio Aguero dakika ya 63 wakati goli la Watford lilifungwa na Andre Gray dakika ya 82.

Msimamo wa EPL ulivyo kwa sasa baada ya kuchezwa game nne January 2 2018.

Niyonzima baada ya Bocco kuipatia ushindi Simba leo

Soma na hizi

Tupia Comments