Tangaza Hapa Ad

AyoTV

VIDEO: Uchambuzi wa Edo Kumwembe baada ya dakika 360 za Pogba Man United

on

Usiku wa Septemba 15 2016 unajua michuano ya Europa League ilichezwa baranni Ulaya watanzania tukamuona Mbwana Samatta akiandika historia mpya katika maisha yake kwa kuwa mtanzania wa kwanza kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Kwa upande wa Man United wao walicheza wakapoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Feyenoord kwa goli 1-0 ugenini, stori ambazo zime trend leo ni kuhusiana na mchezaji ghali zaidi duniani Paul Pogba ikiwa usiku wa jana anakuwa kaichezea Man United jumla ya dakika 360 sawa na mechi nne ila hajatoa assist wala hajafunga goli, Ayo TV imempata mchambuzi wa sok Edo Kumwembe.

“Nafikiri Pogba anacheza kwa presha sana anataka ajaribu kuwadhihirishia watu kuwa anastahili kununuliwa kwa pound milioni 100, kitu ambacho sio kweli sio yeye tu bali hakuna mchezaji mwenye thamani ya pound milioni 100 sema tu sasa hivi hela imekuwa ikitumika tofauti, bado tumpe muda atafanya vizuri Man United lakini sio kuthibitisha kuwa anastahili kununuliwa kwa pound milioni 100”

ALL GOALS: Simba vs AFC Leopard August 8 2016, Full Time 4-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement