Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Jibu la Alikiba alipoulizwa juu ya kushtakiwa kwa kutomhudumia mwanae

on

Staa wa Bongofleva  Alikiba leo May 11, 2017 anafanya mahojiano na Clouds FM ambapo kupitia kipindi cha Leo tena amezungumza kuhusu sakata lililoandikwa kwenye gazeti na kusambaa mtandaoni kuhusu yeye kudaiwa kutomhudumia mtoto wake hivyo mwanamke aliyezaa naye kampeleka mahakamani.

Alikiba alipoulizwa swali hilo amesema habari hizo amesema yeye ameziona kwenye Gazeti ila bado hajapata wito wowote ule wa Mahakama lakini ukweli ni kwamba yeye ana mhudumia mwanae vizuri sana kwani anamsomesha na alimtoa kwenye shule ya kawaida na kumleta shule ya gharama zaidi.

“Nimeona kwenye gazeti lakini bado sijaitwa mahali popote, mtoto namhudumia vizuri hata shule nimemtoa aliyokuwa,  nimempeleka shule nzuri zaidi ya ile tena mara tatu zaidi, Nina watoto watatu wakiume mmoja wakike wawili, mipango ya kupata watoto mwenyezi Mungu atakavyojaalia, watatu au wanne mke wangu hana mtoto”  – Alikiba

ALIYEMCHORA DOGO JANJA TATTOO KAZUNGUMZIA GHARAMA YAKE

Rosa Ree ametuletea Min Super Market aliyowekeza zaidi ya Milioni 30

Soma na hizi

Tupia Comments