Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Ukimuuliza Rage kuhusu jezi ya Mafisango kutumiwa na Mseja jana

on

May 17 2012 taarifa za kifo cha mchezaji wa Simba raia wa Rwanda Patrick Mutesa Mafisango zilianza kusambaa baada ya awali kuripotiwa kuwa amepata ajali na kukimbizwa hospitali lakini madaktari wakathibitisha kuwa amefariki.

Rage

Uongozi wa Simba kwa heshima wakatangaza kuwa jezi namba 30 iliyokuwa inatumiwa na Mafisango wameistafisha kwa heshima haitavaliwa tena na mchezaji yoyote katika club ya Simba SC, hivyo baada ya jana jezi namba 30 kuvaliwa na golikipa wa Simba Mseja.

Golikipa Mseja aliyevaa jezi namba 20 jana

AyoTV imeongea na Rais wa zamani wa Simba SC Ismail Aden Rage na kumuuliza vipi walifuta uamuzi wa kuistafisha jezi namba 30 “sasa hii ungewatafuta viongozi wa sasa ukawauliza mimi pia nimeshituka nilipoona maana sijui hao watu walikuwa wapi wakati ule lakini sisi hatukufuta uamuzi huo ndio maana umeona jezi hiyo ikitumika jana”

Mafisango

Baada ya kipigo “Shida yangu mimi ni msemaji na shabiki wa hii timu”-Manara

Soma na hizi

Tupia Comments