Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Adhabu aliyopewa Patrice Evra kutoka UEFA kwa kumpiga shabiki

on

Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA leo Ijumaa ya November 10 2017 limetangaza kumuadhibu beki wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea Olympique Marseille ya Ufaransa Patrice Evra kwa kosa la kumpiga shabiki wao wakiwa Ureno katika mchezo wa Europa League.

UEFA wamefikia maamuzi hayo kutokana na kitendo cha Patrice  Evra kumpiga teke shabiki wa Marseille ambaye walipishana maneno wakati wachezaji wa Marseille akiwemo Evra wakifanya warm up kuelekea kuanza kwa game hiyo dhidi Vitoria.

Kufuatia kosa hilo UEFA sasa limemfungia Patrice Evra kutocheza mashindano yoyote ya UEFA hadi mwezi June 2018, taarifa hizo zinakuja siku chache baada ya Marseille kuvunja mkataba na Evra kutokana na kufanya kosa hilo la kumpiga shabiki.

Taarifa rasmi kutoka Ubelgiji, Samatta atafanyiwa upasuaji

Soma na hizi

Tupia Comments