Tangaza Hapa Ad

Michezo

Dili jipya la FC Barcelona ambalo litawaingizia zaidi ya Tsh bilioni 500

on

Klabu ya FC Barcelona ya Hispania leo November 16 2016 imeingia mkataba wa udhamini na kampuni ya Rakuten ya Kijapan kwa ajili ya kudhamini timu hiyo kwa miaka minne, Rakuten wameingia mkataba na Barcelona wenye thamani ya pound milioni 200 ambazo ni zaidi ya bilioni 540 za kitanzania.

Mkataba huo wa miaka minne wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi, utaanza kutumika kuanzia mwaka 2017, kuanzia mwaka 2017 usishangae kuona nembo ya Rakuten ikianza kuonekana katika jezi ya FC Barcelona.

3a71df0900000578-3941760-image-m-87_1479303365944

Rakuten ni kampuni ya uuzaji vitu online kupitia tovuti yao na websites yao ni ya 11 kwa uingizaji mapato duniani, kwa jina jingine wanajiita kama “Japan’s Largest Internert Shopping Mall” na kwa mwaka 2015 wamefanikiwa kuingiza pound bilioni 83.5.

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement