Tangaza Hapa Ad

Michezo

Mastaa wa Man United ambao hawatocheza game vs St Etienne

on

Moja kati ya stori za michezo zinazogonga headlines katika ulimwengu wa soka kwa sasa, ni pamoja na hii ya kocha wa Man United Jose Mourinho kuthibitisha kuwa mastaa wake wawili hawatocheza mchezo wao wa 32 bora wa michuano ya Europa League dhidi ya St Etienne.

Kocha Jose Mourinho amethibitisha mbele ya waandishi wa habari kuwa atawapumzisha nahodha wa Man United Wayne Rooney na kiungo wao Michael Carrick katika mchezo dhidi ya St Etienne.

“Rooney na Carrick siwezi kusema kuwa ni majeruhi kwa sababu hapa hatuzungumzii majeruhi ila tunazungumzia matatizo madogo madogo na namna ya kuyatatua hivyo wao watakuwa nje ya uwanja”

Rooney na Carrick

Man United ambayo itacheza dhidi ya St Etienne kesho katika mchezo wa Europa League katika uwanja wa Old Trafford, lakini Mourinho amethibitisha kuwa hatowatumia wachezaji hao kutokana na kushindwa kufanya mazoezi siku ya Jumatano kutokana na kuwa na tatizo la minor muscular.

FULL HD: All goals N’gaya vs Yanga February 12 2017, Full Time 1-5

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement