Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

PICHA: Kilichogundulika baada ya Coutinho kufanyiwa vipimo Barcelona

on

Ni siku moja imepita toka club ya FC Barcelona ya Hispania itangaze kumsajili Mbrazil Philippe Coutinho kutokea Liverpool kwa kiasi kinachotajwa kufikia pound milioni 145, leo Jumatatu ya January 8 2018 zimetoka taarifa za kusikitisha kuhusu staa huyo.

Coutinho ambaye amefanyiwa vipimo vya afya na kusaini mkataba, ndio mchezaji wa pili ghali zaidi duniani baada ya Neymar lakini amegundulika kuwa haweza kucheza kutokana na kukutwa na majeraha ya mguu wake wa kulia hivyo anatarajia kuwa nje ya uwanja kwa wiki tatu kabla ya kupata nafasi ya kucheza game yake ya kwanza.

Kutokana na taarifa hizo ni wazi sasa Coutinho atakosa game ya Copa del Rey dhidi ya Celta Vigo na mechi za LaLiga dhidi ya Real Sociedad, Real Betis na Alaves, hivyo Coutinho anatarajiwa kucheza game yake ya kwanza dhidi ya Espanyol  February 4 2018.

Good news aliyoitangaza Mbwana Samatta January 6 2017

Soma na hizi

Tupia Comments