Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Simon Msuva apiga hat-trick club Bingwa Afrika wakishinda 10-0

on

Mtanzania Simon Msuva anayecheza soka la kulipwa katika club ya Difaa El Jadida ya Morocco Jumamosi ya Febeuary 10 2018 ameichezea timu yake ya El Jadida game yake ya kwanza ya club Bingwa Afrika dhidi ya Sport Bissau E Benfica ya Guinea Bissau.

Msuva alikuwa sehemu ya kikosi cha Difaa El Jadida kilichocheza dhidi ya Sport Bissau E Benfica na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 10-0, kwa upande wa Msuva amefanikiwa kufunga hat-trick katika game hiyo na kuhusika katika upatikanaji wa magoli matatu mengine akitoa pasi mbili za magoli na akisababisha penati.

Hii ndio inakuwa hat-trick ya kwanza ya Simon Msuva kufunga akiwa na Difaa El Jadid, magoli mengine ya Difaa El Jadid yalifungwa na Ahadad aliyefunga magoli matano, N’diaye na Bilal El Megri, sasa Difaa El Jadida watakuwa na kazi nyepesi katika mchezo wa marudiano kwani watakuwa wanahitaji sare tu au hata wakipoteza kwa idadi ya magoli 9-0 watakuwa wamefuzu.

VIDEO: Goli la Juma Mahadhi lililoikosoa Yanga vs St Louis uwanja wa Taifa

Soma na hizi

Tupia Comments