Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Historia imeibeba Simba uwanja wa Sokoine vs Mbeya City

on

Wekundu wa Msimbazi Simba leo walikuwa katika uwanja wa Sokoine Mbeya kucheza mchezo wao wa round ya tisa ya Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara dhidi ya Mbeya City, Simba waliingia katika game hiyo wakiwa na kikosi chao kamili.

Kwa historia Simba ana rekodi nzuri dhidi ya Mbeya City katika uwanja huo wa Sokoine, kwani katika game zao nne za mwisho kukutana toka 2016 uwanja wa Sokoine, Simba imepoteza game mmoja, ushindi game mbili na sare game mmoja, hivyo ushindi wa leo wa goli 1-0 lililofungwa na Shiza Kichuya dakika ya 7 unaendeleza rekodi nzuri.

Ushindi huo sasa umeirejesha Simba kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania bara, baada ya kufanikiwa kufikisha jumla ya point 19 ikiongoza kwa tofauti ya point mbili dhidi ya watani zake wa jadi Yanga, walipo nafasi ya pili kwa kuwa na point 17, Ligi sasa inasimama kwa muda kupisha game za kalenda ya FIFA.

Manara kabeba TV na kuja nayo kwa Waandishi leo kuonyesha Simba inavyoonewa (+video)

Soma na hizi

Tupia Comments