Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Baada ya kurudi uwanjani “Watakula maneno yao”-Ulimwengu

on

Baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na kuuguza majeraha ya goti kwa staa wa timu ya taifa ya Tanzania Thomas Ulimwengu leo Jumatatu ya January 22 2018 ametutangazia good news kwa watanzania kupitia ukurasa wake wa instagram.

Ulimwengu leo amepost video clip ikimuonesha ameungana na wenzake wakiwa mazoezini na kuandika maneno yanayosema “They will eat their Words nashukuru Mungu kwa kuzidi kunipa afya njema” halafu Mbwana Samatta amecomment nakuandika “nakujua ukiwa moto napata woga na hasira utakazorudi nazo keep it up bro”

Thomas Ulimwengu bado hajaweka wazi kama amerudi katika timu yake ya mwanzo ya AFC Eskilstuna ya Sweden au amepata timu mpya ulaya, kwani post yake inaonesha kuwa location yupo Bologna Italy.

VIDEO: Simba ilivyoiadhibu Singida United 4-0 leo, magoli yote yapo hapa

Soma na hizi

Tupia Comments