Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Comment ya Haji Manara baada ya kupewa ushauri na mashabiki wa Yanga

on

Club ya Dar es Salaam Young Africans hivi karibuni ilifanikiwa kupiga hatua na kuingia katika utaratibu mpya wa kuanza kutoa magazine ya club itakayokuwa inatolewa mara nne kwa mwaka.

Yanga wametangaza kuwa watakuwa wanatoa magazine inayohusiana na mambo mbalimbali kuhusu club yao, historia za wachezaji wao na mambo mbalimbali ya club hiyo.

Yanga magazine itakuwa inatolewa mara nne kwa mwaka yaani kila baada ya miezi mitatu, baada ya habari hizo kutoka na magazine hiyo kuanza kusambaa mtaani, mashabiki wanaoaminika kuwa wa Yanga walianza kucomment na kumwambia afisa habari wa Simba Haji Manara afanye utaratibu kama huo kwani Yanga ni mfano wa kuigwa.

Baada ya Haji Manara kuona comment hiyo akajibu hivi “Simba ishavuka huko kwenye makaratasi dunia ya sasa ipo kiganjani sisi tunatoa magazine kila mwezi kwenye app ya club”

“Kijarida cha kufungia maandazi? Nenda kwenye app yetu kaone monthly magazine zetu halafu ndio uniletee hicho kijarida chenu”

Staa wa Simba anayekwenda kufanya majaribio Sweden

Soma na hizi

Tupia Comments