Tangaza Hapa Ad

Michezo

Real Madrid imehitimisha safari ya Sporting CP kucheza 16 bora UEFA

on

Usiku wa November 22 2016 zilichezwa mechi nane za UEFA Champions Leagua hatua ya Makundi, miongoni mwa michezo iliyochezwa usiku wa November 22 ni pamoja na mchezo kati ya Real Madrid dhidi ya Sporting CP klabu iliyomlea Cristiano Ronaldo.

sporting-real-madrid-gareth-bale-joao-pereira_3837911

Mchezo huo ambao ulichezwa katika dimba la Jose Alvande , mashabiki wa Ureno walipata fursa ya kumuona nyota wao Cristiano Ronaldo akihusika kutengeneza goli la kwanza la Real Madrid katika ushindi wa goli 2-1, kipigo hicho kimewafanya Sporting kusubiri mchezo wa kukamilisha ratiba.

skysports-cristiano-ronaldo-cristiano-ronaldo-real-real-madrid_3837921

Sporting CP ikiwa nyumbani katika uwanja wao wenye uwezo wa kuchukua mashabiki zaidi ya elfu 50000, wamekubali kipigo cha goli 2-1 magoli yakifungwa na Raphael Varane dakika ya 29 na Karim Benzema aliyetumia vyema krosi ya Sergio Ramos dakika ya 87, huku Andrien Silva akipachika goli la kufutia machozi kwa Sporting dakika ya 80.

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement