Tangaza Hapa Ad

Michezo

Mipango mipya ya Rais wa FIFA kuhusu klabu Bingwa dunia kuanzia 2019

on

Rais wa shirikisho la soka ulimwengu FIFA Gianni Infantino anapanga kuboresha michuano ya klabu Bingwa dunia kutoka timu 7 hadi timu 32 lengo likiwa ni kuboresha michuano hiyo ili ilete mvuto tofauti na ilivyokuwa sasa.

Gianni Infantino ametoa wazo hilo na kutazamiwa lianze kufanyiwa kazi katika michuano ya klabu Bingwa dunia kuanzia mwaka 2019, michuano hiyo kwa sasa inashirikisha timu 7 kitu ambacho kinatajwa kutokuwa na mvuto na kufanya mshindi iwe rahisi kumtabiri.

screen-shot-2016-11-18-at-7-27-29-pm

Rais huyo anaamini kubadili mfumo huo kutafanya kuongeza mvuto wa mashindano hayo, ambapo karibia kila mara Bingwa wa Ulaya na America Kusini ndio huwa wanakutana fainali, Infantino anaamini mashindano hayo yakiwa yanachezwa kuanzia June 10 hadi June 30 yakishirikisha timu 32 yatakuwa na mvuto.

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement