Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Kwa mwendo huu wa Arsenal na Chelsea, Man City hawezi kukamatika !!!

on

Ligi Kuu England msimu wa 2017/2018 imeendelea tena usiku wa January 3 2018 kwa mchezo mmoja wa London Derby kuchezwa katika uwanja wa Emirates kati ya wenyeji Arsenal dhidi ya Chelsea timu zote hizi zinatokea jiji la London hivyo mvuto wa mchezo huu ulikuwa ni mkubwa.

Arsenal wakiwa nyumbani licha ya kuongoza kwa hali ya umiliki wa mipira kwa asilimia 58 kwa asimilia 42 dhidi ya Chelsea wamejikuta wakilazimishwa sare ya kufungana magoli 2-2, magoli ya Arsenal yakifungwa na Jack Wilshere dakika ya 63 na Hector Bellerin dakika ya 90.

Kwa upande wa Chelsea magoli yao yalifungwa na Eden Hazard kwa penati dakika ya 67 na Marcos Alonso dakika ya 84, sare hiyo sasa inaifanya Chelsea kushuka nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi kwa kufikisha jumla ya point 46.

Nafasi ya pili wapo Man United wana point 47 huku Man City wao wakijikita kileleni kwa kuwa na jumla ya point 62 tofauti ya point 15 na Man United wanaowafuatia, Arsenal wameshuka hadi nafasi ya sita wakiwa na jumla ya point 39.

Kitu Msuva kaandika baada ya kusikia Mahadhi kapiga magoti kuomba msamaha

Soma na hizi

Tupia Comments