Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

PICHA 4: Ni Yanga vs Majimaji leo Feb 14 2018 “Never Give Up”

on

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara club ya Yanga leo iliingia uwanja wa Taifa Dar es Salaam kuwakaribisha wageni wao Majimaji FC kutoka Songea kucheza mchezo wao wa 18 wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2017/2018.

Yanga walikuwa wanaingia katika mchezo dhidi ya Majimaji wakiwa wanarekodi nzuri dhidi yao kwani katika game zao saba zilizopita kabla ya mchezo wa leo walikuwa wamefanikiwa kushinda mara nne na kutoka sare game tatu, game hizo zote tatu za sare ilikuwa Songea.

Kwa bahati mbaya Majimaji leo wameendeleza rekodi yao mbaya dhidi ya Yanga ya kufungwa game za ugenini, mara nyingi kwa miaka ya hivi karibuni Majimaji wamekuwa wakiambulia sare pekee akicheza katika uwanja wake wa nyumbani Songea, leo Majimaji imekubali kipigo kingine cha magoli 4-1.

Magoli ya Yanga yakifungwa na Papy Tshishimbi aliyefunga mawili dakika ya 20 kwa penati na dakika ya 84, Obrey Chirwa dakika ya 30 na Emmanuel Martin aliyefunga dakika ya 44 wakati Majimaji wao wakiambulia goli la kufutia machozi dakika ya 56 kwa mkwaju wa penati uliyopigwa na Marcel Kaheza.

Baada ya kufunga Chirwa akaonesha tisheti yake ya ndani yenye ujumbe ‘Never Give Up’ Chirwa aliingia kwenye headlines hivi karibuni baada ya mfululizo wa kukosa penati.

Msimamo wa VPL baada ya game ya leo.

VIDEO:Magoli ya Simba walivyorudi kimataifa leo vs Gendermarie Full Time 4-0

Soma na hizi

Tupia Comments